Mradi wa upanuzi wa kituo cha umeme nchini Zambia uliotekelezwa na kampuni ya China waanza kuzalisha umeme
2023-02-17 08:44:21| CRI

Mradi wa upanuzi wa kituo cha umeme wa jua kilichoko Kitwe, mkoa wa Copperbelt nchini Zambia uliotekelezwa na Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya Sinohydro ya China, umeanza rasmi kuzalisha umeme Februari 15.

Akizungumza katika hafla hiyo, rais wa Zambia Hakainde Hichilema amesema, upanuzi wa kituo hicho una umuhimu mkubwa, kwani Zambia haitaendelea kusumbuliwa na kukatika kwa umeme. 

Mradi huo unatarajiwa kuzalisha umeme zaidi ya saa za kilowati milioni 56 kwa mwaka.