Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) jana imesema, idadi ya raia walioathiriwa na matumizi ya mabavu nchini Sudan Kusini imeongezeka kwa kasi mwishoni mwa mwaka 2022, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2021.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Tume hiyo, idadi ya raia walioathirika na matumizi ya mabavu kuanzia mwezi Oktoba hadi Desemba mwaka 2022 iliongezeka kwa asilimia 87 kuliko wakati kama huo mwaka 2021. Matukio ya kutekwa nyara na unyanyasaji wa kijinsia pia yaliongezeka sana ikilinganishwa na mwaka 2021.