Kaimu Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) Antonio Pedro amesema, masoko ya kaboni yanatoa fursa kubwa kwa nchi za Afrika kutumia vizuri hifadhi kubwa ya rasilimali zilizoko katika bara hilo.
Pedro amesema hayo katika taarifa yake iliyotolewa kabla ya mkutano wa kila mwaka wa biashara wa Afrika unaoandaliwa kwa pamoja na UNECA na Benki ya Uagizaji na Uingizaji ya Afrika (Afreximbank) unaolenga kufanya majadiliano kati ya wafanyabiashara wa Afrika na viongozi wa kisiasa na watungasera kuhusu kutimiza Ajenda ya mwaka 2063 na Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Afrika ina kiasi kikubwa cha kaboni kilichohifadhiwa katika mfumo wake wa ikolojia, huku misitu ya Kongo ikiwa na uwezo wa kufyonza tani karibu bilioni 1.2 za hewa ya kaboni kila mwaka.