Waziri Mkuu wa China Bw. Li Keqiang amempongeza Manuela Roka Botey kwa kuapishwa kuwa waziri mkuu mpya wa Guinea ya Ikweta.
Katika salamu hizo, Bw. Li amesema, China na Guinea ya Ikweta ni marafiki wa jadi, zinaaminiana kisiasa kwa uthabiti na kufanya ushirikiano wenye manufaa katika nyanja mbalimbali. Amesema China inatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kupenda kushirikiana na Guinea ya Ikweta kusukuma mbele uhusiano wa pande zote wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili upande ngazi ya juu.