Kiplimo awa bingwa wa mbio za nyika za 2023
2023-02-20 15:09:28| cri

Mwanariadha wa Uganda Jacob Kiplimo Jumamosi alishinda medali ya dhahabu katika taji la Dunia la Mbio za Nyika 2023 nchini Australia.

Kiplimo alitumia dakika 29 sekunde 17 kuzunguka njia yenye urefu wa kilomita 10 katika Mlima Panorama huko Bathurst, kaskazini-magharibi mwa Sydney -- inayojulikana zaidi kama mojawapo ya njia zenye changamoto kubwa zaidi za mbio za magari duniani. Alivuka mstari wa mwisho kwa akimzidi Berihu Aregawi wa Ethiopia kwa sekunde tisa mbele huku Mganda mwenzake Cheptegei akitwaa shaba.

Cheptegai anayeshikilia rekodi ya dunia ya mita 5,000 na 10,000 -- alikuwa akitetea taji aliloshinda miaka minne iliyopita mjini Aarhus, Denmark wakati Kiplimo alipotwaa fedha. Bingwa wa mataji mawili ya Jumuiya ya Madola Kiplimo sasa anashikilia mataji ya dunia ya Mbio za Nyika na Nusu Marathon.