Tamasha la Maonesho ya Filamu za Documentary la China kuhusu “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lazinduliwa rasmi
2023-02-20 15:06:55| cri

Tamasha la Maonesho ya Filamu za Documentary la China kuhusu “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ambalo liliandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG likishirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje, na Wizara ya Utamaduni na Utalii, leo limezinduliwa rasmi mtandaoni, ambapo watu mashuhuri zaidi ya 50 kutoka serikali na mashirika ya vyombo vya habari kutoka nchi na sehemu zaidi ya 40 walitoa hotuba kwa video wakilitakia mafanikio tamasha hilo.

Huu ni mwaka wa 10 tangu rais wa China Xi Jinping atoe pendekezo la kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Katika tamasha hilo, filamu za documentary zaidi ya 60 zinazoonesha hadithi za maendeleo na mawasiliano ya kirafiki za nchi zilizojiunga na Pendekezo hilo, ambazo zilitayarishwa na kutengenezwa kwa lugha mbalimbali na CGTN zitaoneshwa kwa watazamaji kote duniani.

Katika hafla ya uzinduzi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang, Waziri wa Utamaduni na Utalii Hu Heping na Mkuu wa CMG Shen Haixiong walitoa hotuba na kuzindua kwa pamoja tamasha hilo.