Pande husika za Sudan zasaini ratiba ya miaka miwili ya utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Juba
2023-02-20 08:54:29| CRI

Serikali ya mpito ya Sudan na makundi kadhaa ya upinzani chini ya Kundi la kimapinduzi la Sudan (SRF) wamesaini hati inayohusu ratiba ya miaka miwili ya utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Juba.

Masuala muhimu yanayotajwa kwenye hati hiyo ni pamoja na upangaji wa mambo ya usalama katika jimbo la Darfur, South Kordofan na Blue Nile na mgawanyo wa mali na madaraka kati ya makundi ya upinzani yaliyoko katikati na kaskazini mwa nchi hiyo.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ambaye ni mpatanishi kwenye kusaini kwa makubaliano ya amani kati ya pande hizo, amesema upangaji huo mpya ni kwa ajili ya kuhimiza mazungumzo kati ya pande mbalimbali husika za Sudan na kuifanya nchi hiyo ielekee amani ya kudumu.