Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Zambia Bw. Stanley Kasongo Kakubo na kusema China iko tayari kushirikiana na Zambia kuimarisha ushirikiano kati yao.
Bw. Qin Gang amesema China inapenda kushirikiana na Zambia kwa kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili na iko tayari ya kuimarisha ushirikiano na Zambia katika sekta mbalimbali chini ya pendekezo la “ Ukanda Mmoja, Njia Moja” na mfumo wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, na China inakaribisha bidhaa nyingi zaidi zenye ubora wa juu za Zambia kuingia kwenye soko lake.
Bw. Kakubo ameshukuru uungaji mkono wa China katika maendeleo ya Zambia kwa miaka mingi, huku akitarajia kuwa ushirikiano na urafiki kati ya nchi hizo mbili utaendelea kuimarika.