Kamati Kuu ya 20 ya CPC kufanya mkutano wa pili wa wajumbe wote
2023-02-21 16:38:28| CRI

Mkutano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 mwezi huu mjini Beijing.

Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano wa Kamati Kuu ya CPC uliofanyika leo chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu wa Kamati hiyo, Xi Jinping.