Manowari za kikosi cha 42 za jeshi la majini la China, ikiwemo manowari ya Destroyer Huainan, manowari ya makombora Frigate Rizhao na meli ya ugavi, ziliwasili juzi katika Bandari ya Richards Bay nchini Afrika Kusini, kwa ajili ya kushiriki katika luteka ya pamoja ya baharini kati ya China, Russia na Afrika Kusini.
Jeshi la majini la Afrika Kusini lilifanya sherehe kubwa ya kuzikaribisha.
Luteka hiyo ambayo inafanyika katika pwani ya mashariki na anga kutoka Durban hadi Richards Bay, ni ya pili ya pamoja ya baharini kufanywa na majeshi ya majini ya nchi hizo tatu tangu mwaka 2019.