Rais Xi apongeza kuanzishwa kwa taasisi ya kufundishana kati ya staarabu za China na Ugiriki
2023-02-21 08:37:28| CRI

Rais Xi Jinping wa China amejibu barua aliyoandikiwa hivi karibuni na prof. Stelios Virvidakis wa Chuo kikuu cha Athens na wasomi wengine wanne wa Ugiriki, akitoa pongezi kutokana na kuanzishwa kwa Kituo cha Staarabu za Kale za China na Ugiriki.

Kwenye barua yake, Rais Xi amesisitiza umuhimu mkubwa wa kihistoria na kwa zama za leo kwa nchi hizo mbili kuanzisha kituo hicho, ambacho kinalenga kuhimiza kuwasiliana na kufundishana kati ya staarabu zao na kuhimiza maendeleo ya staarabu za nchi mbalimbali.

Rais Xi amesema, ili kusukuma mbele maendeleo ya jamii ya binadamu na kujenga kwa pamoja jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja, watu wote wanapaswa kuelewa kwa kina na kushikilia asili na undani wa staarabu tofauti na kuzitumia kunufaisha watu wa vizazi vya sasa na binadamu wote.