Algeria yatangaza kutenga dola bilioni 1 kwa ajili ya maendeleo ya Afrika
2023-02-21 19:52:43| cri

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune amesema nchi yake itatenga dola bilioni moja ili kufadhili miradi ya maendeleo katika bara zima kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mshikamano na Maendeleo la Algeria.

Shirika rasmi la habari la APS limesema uamuzi wake ulitangazwa katika hotuba iliyosomwa na Waziri Mkuu Aymen Benabderrahmane katika mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia, siku ya Jumapili. Zingatio litakuwa zaidi kwenye "miradi jumuishaji au ile ambayo inaweza kuchangia katika kuharakisha maendeleo barani Afrika".

Tebboune alisema mtazamo wa shirika hilo ulitokana na imani ya Algeria kwamba "usalama na utulivu barani Afrika vinahusiana na maendeleo".