Rais Biden afanya ziara ya ghafla mjini Kiev wakati maandamano ya kupinga vita yakiendelea nchini Marekani
2023-02-21 08:55:23| CRI

Rais Joe Biden wa Marekani amefanya ziara ya ghafla mjini Kiev siku moja baada ya maandamano ya kupinga sera ya mambo ya nje ya Marekani inayochochea vita na ushiriki wa Marekani kwenye migogoro mbalimbali duniani.

Kwenye ziara yake Rais Biden amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Volodymyr Zelensky kuhusu hali ya mapambano kwenye mstari wa mbele, na pia ametangaza msaada zaidi wa dola za kimarekani milioni 500, mbali na dola bilioni 50 ambazo tayari zimeahidiwa.

Ziara ya Rais Biden imefanyikia siku nne kabla ya kutimia mwaka mmoja tangu mgogoro huo uanze, ikiwa na lengo la kuonesha mshikamano na Ukraine.