Mkutano wa 43 wa kawaida wa baraza la mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC unaofanyika huko Burundi, utapitia tena ripoti ya tume ya usimamizi kuhusu ombi la uanachama wa Somalia katika jumuiya hiyo.
Taarifa iliyotolewa jana na makao makuu ya Jumuiya ya EAC huko Arusha, imesema tume hiyo imemaliza ripoti yake baada ya kufanya ziara nchini Somalia kuanzia Januari 25 hadi Februari 3.
Kujiunga kwa Somalia katika jumuiya ya EAC kutafanya idadi ya ujumla ya nchi wanachama kuongezeka hadi nane. Hivi sasa Jumuiya hiyo inaundwa na Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na Uganda.