Kama Marekani itaiga inachofanya China barani Afrika, sio tu itajivunia heshima bali pia haitapata inachotaka
2023-02-22 14:19:15| CRI


Siku chache baada ya waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang kumaliza ziara yake ya mwaka mpya barani Afrika, waziri wa fedha wa Marekani na balozi wa nchi hiyo kwenye Umoja wa Mataifa walianza ziara zao barani humo mmoja baada ya mwingine. Na imeeleweka wazi kuwa lengo kuu la ziara hizo ni "kukabiliana na ushawishi wa China barani Afrika." Lakini wanaweza wasitambue kuwa kama Marekani inajaribu kuiga inachofanya China barani Afrika, sio tu inajivunjia heshima bali pia haitapata inachotaka.

Siku hizi, "nguvu ya uongozi duniani" iliyo nayo Marekani inapungua kwa kasi, hali ambayo inaweza kuonekana kwenye majibu ya upande wa Afrika. Katika siku ya pili baada ya waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen kuanza ziara yake barani Afrika, serikali ya Afrika Kusini ilitangaza kuwa itafanya mazoezi ya kijeshi na China na Russia katika bahari ya nchi hiyo mwezi Februari. Baadaye waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Bibi Naledi Pandor, alipokutana na Yellen alisema moja kwa moja, “tunakaribisha ziara za maofisa waandamizi kutoka Marekani, lakini tunaitumai Marekani itaondoa vikwazo vya upande mmoja dhidi ya nchi za Afrika.” Ni wazi kuwa Afrika Kusini, nchi yenye nguvu kubwa zaidi kiuchumi barani Afrika haitaki kuipa Marekani heshima yoyote. Halisi ni kuwa tangu rais Biden aingie madarakani, nchi za Afrika zimetambua wazi hila za Marekani kuharibu uhusiano kati ya China na Afrika, ambazo matokeo yake ni madogo. Hii ni kutokana na sababu tatu zifuatazo:

Kwanza, mtindo wa ushirikiano unaotolewa na China unaendana na maslahi ya maendeleo ya nchi za Afrika. Kwa muda mrefu, Marekani imekuwa ikiichukulia Afrika kama “chombo” chake, na hata mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama wa Marekani Bw. Jake Sullivan aliitambulisha Afrika kama "mshirika mkuu wa siasa za kijiografia", kwa mfano kwenye mgogoro kati ya Russia na Ukraine, Marekani inatumai nchi za Afrika kuilaani Russia, la sivyo zitaadhibiwa. Lakini China nayo siku zote imekuwa ikisisitiza ushirikiano wa kunufaishana kati yake na Afrika na kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Pili, China inaweza kuleta manufaa halisi kwa Afrika. Kutoka Reli ya TAZARA iliyojengwa takriban nusu karne iliyopita hadi Kituo cha Afrika CDC kilichozinduliwa mwezi uliopita, "Jumuiya ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja" haijawahi kuwa kauli mbiu ya maneno matupu. Lakini Marekani ni tofauti. Kutoka kwa mpango wa Obama wa "Power Africa" hadi mpango wa "Jenga Upya Ulimwengu Bora" wa Biden, Marekani imetoa mapendekezo mengi kuhusu Afrika, lakini utekelezaji wao ni mbaya. Kwa hiyo, nchi nyingi za Afrika zinachagua ushirikiano halisi wa China badala ya keki ambazo Marekani inaendelea kuchora.

Tatu, Marekani haina msimamo endelevu kuhusu Afrika kama ilivyo China. Tofauti na utawala wa rais aliyepita Donald Trump, serikali ya Biden sasa inasema "itaweka kila kitu barani Afrika." Lakini je, "Marekani imerejea" leo, hakuna anayejua kama Marekani itaondoka tena wakati rais ajaye wa Marekani atakapoingia madarakani. Kinyume chake, Waziri wa Mambo ya Nje wa China ametembelea Afrika katika ziara ya mwaka mpya kwa miaka 33 mfululizo, na China pia imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 13 mfululizo, ambapo urari wa biashara kati ya China na Afrika unaendelea kukaribia uwiano  mwaka hadi mwaka. Ni nani kati ya China na Marekani ambaye ni mwaminifu zaidi kwa Afrika, hii imejulikana kupitia vitendo halisi.

Ni jambo la kufurahisha kuona uwepo wa China barani Afrika umekuwa ni msukumo kwa Marekani kurudi barani Afrika. Lakini, waziri wa mambo ya nje wa China Qin Gang pia alisema katika ziara yake ya hivi karibuni barani Afrika kwamba Afrika haipaswi kuwa uwanja wa michezo wa nchi kubwa. Kauli hii ni kuikumbusha Marekani kwamba Marekani kuongeza ushirikiano na Afrika hakupaswi kuilenga China, la sivyo inayoumia ni Afrika.