Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amesema jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuongeza misaada kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ili kuisaidia kufikia amani na usalama wa kudumu katika kipindi nyeti cha mpito kwake cha kutoka ulinzi wa amani hadi ujenzi wa amani.
Balozi Dai amesema China inaunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika kulinda amani kwa mujibu wa sheria na kutaka pande husika zisitishe matumizi ya mabavu. Ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuheshimu mamlaka ya nchi hiyo, na kuisaidia kuhakikisha uchaguzi wake wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu ufanyike kwa utulivu.
Pia ametaka vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama kwa nchi hiyo vinavyoathiri uwezo wake wa ulinzi viondolewe.