Marekani ndio chanzo kikubwa cha silaha za vita nchini Ukraine
2023-02-22 10:22:36| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wan Wenbin amesema kuna ushahidi tosha kuwa Marekani ni chanzo cha matatizo na wala sio mlinzi wa amani duniani.

Akitolea mfano kuwa Marekani ni chanzo kikubwa cha sialaha za vita nchini Ukraine, Bw. Wang amesema ni jana tu Marekani ilitangaza kuipatia Ukraine msaada wa kijeshi wenye thamani ya dola milioni 500. Amesema inafanya watu washangae kwamba Marekani inataka kufanya nini inapotoa madai ya uongo kuwa China inatoa silaha, na kama Marekani inaona busara kuutangazia ulimwengu kwamba inataka amani ilhali bado imekaa na kuangalia sekta yake ya ulinzi ikijipatia pesa kwa njia za udanganyifu.

Wang amesisitiza kuwa ushirikiano wa kina na kimkakati kati ya China na Russia umejengwa kwa msingi wa kutokuwa na muungano, kutokuwa na makabiliano na kutolenga upande wowote wa tatu, ambao upo ndani ya haki ya mamlaka ya mataifa yoyote mawili yaliyo huru.