Waziri wa Mambo ya Nje asema China itaendelea kulinda amani duniani
2023-02-22 10:22:02| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amesema China kamwe haitatafuta utawala, upanuzi au ushawishi wa pande mbalimbali, ama kushiriki kwenye mbio za silaha bali itabaki kuwa mlinzi wa amani duniani.

Kauli hiyo ameitoa wakati akihutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa Kongamanao la Lanting juu ya Pendekezo la Usalama Duniani GSI, ambalo ni mpango wa China wa kutatua Changamoto za Usalama, wakati ambapo China imetoa rasmi “Waraka wa Dhana ya Pendekezo la Usalama Duniani.”

Bw. Qin amesema GSI inashikilia mtazamo wa usalama wa pamoja, wa kina, ushirika na endelevu, kutafuta malengo ya muda mrefu ya kujenga jumuiya ya usalama na kutetea njia mpya ya usalama kupitia mazungumzo badala ya makabiliano, ushirikiano badala ya kuwa na makundi, na kunufaishana badala ya kushinda upande mmoja na mwingine usishinde.

Bw. Qin vilevile amesema usalama ni haki ya nchi zote, na sio upendeleo wa baadhi ya nchi, wala kuamuliwa na nchi moja. GSI inalenga kuhudumia maslahi ya wote na kulinda utulivu wa wote. Inakuza mahitaji ya umoja na ushirikiano wa jamii ya kimataifa.