Russia yasitisha ushiriki wake katika mkataba mpya wa START
2023-02-22 10:18:51| CRI

Rais Vladimir Putin wa Russia ametangaza kuwa Russia haijiondoi bali inasitisha ushiriki wake kwenye Mkataba Mpya wa Kupunguza Silaha za Kimkakati (New START) iliofikia na Marekani.

Shirika la NATO lilidai mapema mwezi huu kwamba, Russia "irudi kwenye utekelezaji" wa New START na kuruhusu ukaguzi wa vifaa vyake vya nyuklia. Putin alisema, huo unaonekana kama aina fulani ya upuuzi katika makabiliano ya leo.

Rais Putin ameongeza kuwa nchi yake imepata habari kwamba viongozi kadhaa wa Marekani wanafikiria kufanya majaribio ya silaha za nyuklia ili kuunda aina mpya za silaha za nyuklia.