Misri yatarajia kuvutia uwekezaji zaidi kutoka China
2023-02-22 08:36:10| CRI

Maofisa na viongozi wa biashara kutoka Misri wamesema kwenye semina moja iliyofanyika hivi karibuni mjini Cairo kuwa Misri inatarajia kuvutia uwekezaji zaidi kutoka China kupitia kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini humo.

Semina ya Wajasiriamali wa China na Misri iliyoandaliwa Jumatatu na Shirikisho la Wafanyabiashara la Misri, ilihudhuriwa na balozi wa China nchini Misri Liao Liqiang na wajumbe wapatao 130 wa kampuni, taasisi za kifedha na mashirika ya kuhimiza uwekezaji kutoka nchi hizo mbili.

Akiongea kwenye semina hiyo, Ofisa mtendaji mkuu wa Mamlaka Kuu ya Uwekezaji na Maeneo ya Biashara Huria ya Misri Bw. Hossam Heiba amepongeza ushirika mpana na wa kina wa kampuni za China kwenye soko la Misri na katika ujenzi wa miradi mbalimbali nchini humo, na vilevile amesifu mchango wao mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii na uendelezaji wa viwanda nchini Misri.