Xi asisitiza utafiti wa kimsingi wa kujitegemea katika sayansi na teknolojia
2023-02-22 15:04:09| CRI

Rais Xi Jinping wa China amehimiza kuimarishwa kwa utafiti wa kimsingi ili kuongeza nguvu na kujitegemea katika sayansi na teknolojia.

Xi alisema hayo alipoongoza semina ya tatu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 20 ya CPC jana Jumanne mchana. Aidha alisema kuimarisha utafiti wa kimsingi ni hitaji la dharura ili kuweza kujiimarisha zaidi na kuwa na nguvu katika sayansi na teknolojia, na ndio njia pekee ya kujijenga kuwa nchi yenye nguvu zaidi katika sayansi na teknolojia.