Ofisa wa afya wa Umoja wa Afrika apongeza ushirikiano kati ya China na Afrika
2023-02-22 09:23:31| CRI

Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia afya, mambo ya kibinadamu na maendeleo ya kijamii Bi. Minata Samate Cessouma amepongeza uhusiano wa kiwenzi kati ya China na Afrika, huku akisisitiza ushirikiano wenye ufanisi katika sekta ya afya.

Bi. Cessouma amesema China ni mwenzi mkubwa wa Afrika na matumaini yaliyopo ni kuendeleza ushirikiano na China, kubadilishana uzoefu na China na kuona jinsi wanavyoweza kutimiza Ajenda 2063 ya Afrika.

Kamishna huyo ametoa mwito kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika kupitia msaada wa majukwaa ya ushirikiano, ikiwemo baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC.