Tamthilia ya kichina “The Knockout” yajizolea umaarufu mkubwa
2023-02-22 14:22:16| CRI


Siku hizi, tamthilia ya kichina “The Knockout” inayosimulia vita kati ya uovu na uadilifu imendelea kupata umaarufu mkubwa, na hadi sasa idadi ya watazamaji wa tamthilia hiyo katika China bara pekee imezidi milioni 320.

Utayarishaji bora na ustadi mkubwa wa waigizaji ndio sababu zinazofanya tamthilia hiyo kuvuma sana, lakini cha muhimu zaidi ni kwamba tamthilia hiyo inahusu suala la ufisadi serikalini ambalo linahusisha maslahi muhimu ya watu wa kawaida, na pia kuonyesha kuwa vita vikali dhidi ya ufisadi nchini China vimekita mizizi katika mioyo ya watu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Hapa China, kupambana na ufisadi sio mada inayopigwa marufuku kuzungumzwa na umma. Msemo wa kale wa kichina unasema, "Kuporomoka kwa nchi kunasababishwa na viongozi waovu", ikimaanisha kuwa ufisadi ni tatizo ambalo linaweza kusababisha kupinduliwa kwa utawala. Katika nchi yoyote, iwapo kuna madaraka, kuna uwezekano wa kutokea kwa ufisadi. Kuwa na ujasiri wa kujifanyia mapinduzi ni sifa kuu kiliyo nayo Chama cha Kikomunisti cha China CPC, tofauti na vyama vingine vya kisiasa katika nchi nyingine. Wakati huo huo, watu wa China wamepewa haki ya kufuatilia na kutathmini jinsi maofisa wanavyotumia madaraka yao, si tu kwa sababu watu wa kawaida wana sauti kubwa zaidi, lakini cha muhimu zaidi ni kuwa kupambana na ufisadi kunahusiana na mioyo ya watu na ni suala kubwa zaidi la kisiasa nchini China.

Hapa China, kupambana na ufisadi sio ilani ya uchaguzi. Katika baadhi ya nchi, vita dhidi ya ufisadi vimekuwa propaganda ya wagombea urais wakati wa kampeni zao za uchaguzi, lakini mara nyingi hubaki kuwa "kauli mbiu" tu baada ya kuchukua wadhifa. Hata katika nchi kama Marekani, fedha nyingi zinatiririka katika uchaguzi mkubwa, jambo ambapo inaonesha kuwa huu ni mfano halisi wa ufisadi mkubwa. Katika miaka kumi iliyopita, idara za ukaguzi na usimamizi wa nidhamu za ngazi mbalimbali nchini China zimechunguza kesi zaidi ya milioni 4.5, na kuwaadhibu zaidi ya watu milioni 4.4 kwa njia mbalimbali. Hii inadhihirisha kikamilifu kwamba "ukali" ndio sifa kuu ya vita dhidi ya ufisadi nchini China. Chama cha Kikomunisti cha China hakijitafutii maslahi yake yoyote binafsi, kwa hivyo bila kujali ni nani anayekiuka nidhamu ya Chama na sheria za nchi, hatasamehewa.

Hapa China, vita dhidi ya ufisadi haipiti tu kama upepo, wala sio mapambano ya kisiasa. Ufisadi na vita dhidi ya ufisadi ni mapambano ya muda mrefu ambayo hayawezi kufanikiwa kabisa ndani ya muda mfupi. Hadithi ya tamthilia “The Knockout” inaanzia wakati maofisa wa ngazi ya juu wanaamua kupitia tenakesi zilizokamilishwa. Hivi sasa, utaratibu wa kupambana na ufisadi kimsingi umekamilika nchini China, lakini uwezo wa kudhibiti ufisadi bado unahitajika kuboreshwa. Kimsingi, China bado ni jamii inayozingatia mahusiano ya watu, si jambo rahisi kwa maofisa waliozaliwa na kukua katika mazingira hayo ya kijamii kuwa na fikrasio tu ni pamoja na "kutothubutu kufanya ufisadi" na "kutoweza kufanya ufisadi", lakini pia "kutotaka kufanya ufisadi" mioyoni mwao ndani ya muda mfupi. Katika suala hili, pamoja na kuongeza adhabu na kuongeza usimamizi wa madaraka, China pia inajitahidi kuongeza mwamko wa maofisa wa chama kuwatumikia wananchi kwa moyo wote, kuelewa kwa kina maana ya “maji yanaweza kubeba boti, lakini pia yanaweza kuipindua”.

Tamthilia ya "The Knockout" inawawezesha watu wa kawaida wa China kuona kwamba bila kujali hali ni ngumu kiasi gani na jinsi nguvu za ufisadi na uovu zinavyoenea kwa nguvu, kuunda mazingira ya kijamii yenye haki na usawa ni kipaumbele cha juu cha kazi kwa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali. Je, watazamaji wanawezaje kutopenda ahadi hiyo ya dhati?