Rais Xi aamuru juhudi zote za uokoaji kufuatia mgodi wa makaa ya mawe kuporomoka Mongolia ya Ndani
2023-02-23 08:48:06| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametaka juhudi zote zifanywe kuwatafuta na kuwaokoa wafanyakazi ambao hawajulikani walipo na kuwatibu wale waliojeruhiwa baada ya mgodi wa makaa ya mawe kuporomoka katika mji wa Alxa mkoani Mongolia ya Ndani.

Rais Xi ametoa agizo hilo kufuatia kutokea kwa ajali hiyo, akihimiza juhudi za kuhakikisha usalama wa maisha na mali ya wananchi, na kudumisha utulivu wa jamii kwa ujumla.

Mpaka sasa ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wawili, watu sita wamejeruhiwa na wengine 53 hawajulikani walipo.

Rais Xi ametaka juhudi kufanywa kubaini chanzo cha ajali hiyo haraka iwezekanavyo na kuwawajibisha watu waliohusika, na kuondoa mianya yoyote kwenye usimamizi.