Kamisheni ya Usimamizi wa Majanga ya Ethiopia imetangaza kuwa zaidi ya tani 157,000 za chakula zimesambazwa kwa watu walioathirika na machafuko kaskazini mwa nchi hiyo.
Shirika la Utangazaji la Fana (FBC) limemnukuu mkurugenzi wa mahusiano ya umma wa kamisheni hiyo Bw. Debebe Zewdie akisema raundi ya pili ya msaada wa dharura wa chakula inasambazwa kwa watu milioni 21.2 walioathirika na machafuko na ukame.
Ofisa huyo amesema usambazaji wa msaada huo wa chakula uliotolewa na serikali ya Ethiopia na mashirika ya kibinadamu umekamilika kwa asilimia 92.
Bw. Zewdie amesihi mwitikio wa dharura kutoka wadau wa serikali, binafsi na mashirika ya kibinadamu, akisisitiza kuwa bado kuna mamilioni ya watu wanaohitaji msaada wa dharura wa chakula kote nchini humo.