Msomi wa Mali: Historia ya uhusiano wa nje ya Marekani inajaa uongo na mabavu
2023-02-24 14:53:44| CRI

Kitendo cha Marekani kutoa taarifa zisizo za kweli kuhusu kile inachokiita “puto la kijasusi” ili kuipaka matope China kimezua upinzani mkali. Mtaalamu wa masuala ya kimataifa kutoka Mali Prof. Yoro Diallo alipohojiwa hivi karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, ameitaja Marekani ilivyotuma ndege ya kisasa ya kivita kutungua puto la hali ya hewa la China kwa kombora, kama “mtu asiye na akili kuua inzi kwa kutumia nyundo”. 


Prof. Diallo ambaye alikuwa mwanadiplomasia wa Mali nchini China na sasa ni mtafiti mwandamizi katika Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, amesema, puto la matumizi ya kiraia la China kuingia kwenye anga ya Marekani ni tukio pekee lisilotarajiwa ambalo lilitokana na nguvu isiyodhibitika, lakini Marekani ilitoa taarifa zisizo za kweli kuhusu “puto la kijasusi”, kitendo ambacho kimekumbusha jinsi Marekani ilivyotunga uongo wa “sabuni ya unga” kama kisingizio cha kuanzisha vita dhidi ya Iraq. Amesema, historia ya uhusiano wa nje ya Marekani inajaa uongo na mabavu, na Marekani imeanzisha vita na uingiliaji wa kijeshi mara kwa mara dhidi ya nchi nyingine kwa msingi wa uongo, hatua za upande mmoja na siasa ya umwamba. Mgogoro wa Ukraine unaozidi kupamba moto hadi leo, hauko mbali na uchochezi wa nchi za Magharibi zinazoongozwa na Marekani. 


Prof. Diallo anaona, hata Marekani ikiichafua China kiasi gani, haitabadilisha mtazamo wa nchi za kusini hasa zile za Afrika kuhusu China, kwa kuwa wanajua wazi nani ni rafiki na mwenzi wa kweli.