Rais Xi Jinping wa China asisitiza kushikilia na kueneza moyo wa Lei Feng
2023-02-24 14:31:08| cri

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza umuhimu wa kuelewa kwa kina moyo ya Lei Feng ili moyo huo uangaze zaidi katika enzi mpya.

Rais Xi amesema hayo alipotoa maagizo muhimu ya kutekeleza zaidi shughuli za kujifunza kutoka kwa marehemu Lei Feng, aliyekuwa askari wa kawaida nchini China ambaye aliwasaidia wengine bila ubinafsi.

Rais Xi amebainisha kuwa 2023 ni mwaka wa 60 tangu wanamapinduzi wa kizazi kikongwe, ikiwa ni pamoja na Mao Zedong, kuandika maandishi kwa ajili ya komredi Lei Feng. Amesema shughuli za kujifunza kutoka kwa Lei Feng zimeendelezwa kwa kiasi kikubwa katika miongo sita mfululizo iliyopita.

Rais Xi ameongeza kuwa jina la Lei Feng limekuwa maarufu nchini China, na matendo yake yanavutia umma, moyo wake umekuza akili za Wachina kutoka kizazi hadi kizazi.