China yataka suluhisho la kisiasa kwa mgogoro wa Ukraine
2023-02-24 21:33:03| cri

Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amesema, uwezeshaji wa kusimamisha mapigano ni kipaumbele kikubwa na ufunguo wa suluhisho la kisiasa la mgogoro wa Ukraine.

Akizungumza katika Mkutano Maalum wa Dharura wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine uliofanyika jana, Balozi Dai Bing amesema, historia inafundisha kuwa, migogoro yoyote inaweza kutatuliwa kwa amani, na kwamba mlango wa suluhisho la kisiasa hauwezi kufungwa. Amesema China inaunga mkono Russia na Ukraine kurejesha majadiliano ya moja kwa moja haraka iwezekanavyo, kujadili masuala halali ya kila upande, kutafuta njia mbadala, na kutoa nafasi ya kumalizika mapema kwa mgogoro huo na kujenga upya amani.

Amesema pande zinazopingana zinapaswa kushikilia kidhabiti sheria ya kimataifa ya kibinadamu, kukwepa kushambulia raia na miundombinu ya kiraia, kulinda wanawake, watoto na wahanga wengine wa mgogoro, na kuheshimu haki za msingi za wafungwa wa kivita.