Ujumbe wa Shirika la Utalii Duniani wahudhuria hafla ya kufunguliwa kwa utalii China
2023-02-24 09:09:04| CRI

Ujumbe kutoka Shirika la Utalii duniani WTO umehudhuria hafla ya kufunguliwa tena kwa sekta ya utalii nchini China baada ya janga la COVID-19, ujumbe ambao umesafiri kutoka mjini Madrid, Hispania hadi katika mji wa Hangzhou, mkoani Zhejiang.

WTO imesema kufunguliwa kuwa utalii nchini China kunakamilisha sehemu iliyobaki katika kufufua sekta ya utalii baada ya kukumbwa na msukosuko mkubwa kufuatia janga la COVID-19.

Mwaka 2019 kabla ya janga hilo China ilikuwa soko kubwa zaidi la utalii duniani, ambapo watalii wa China wapatao milioni 166 walifanya safari katika nchi mbalimbali na kutumia dola za kimarekani bilioni 270 ambazo zilisaidia nchi mbalimbali zinazoendelea.

Kwa mujibu wa WTO jumla ya dola za kimarekani trilioni 3 zilipotea duniani kati ya mwaka 2020 na 2022 kutokana na janga la COVID-19.