Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi amezindua mkutano wa kwanza wa utalii huko Zanzibar, unaolenga kuwaunganisha wadau wa sekta ya utalii na wawekezaji wa ndani, Afrika Mashariki na kimataifa katika sekta hiyo.
Rais Mwinyi amesema kuwa sekta ya utalii ya Zanzibar ina mchango mkubwa kwani inachangia asilimia 30 ya pato la taifa, na serikali ya Zanzibar imeongeza kuchukua hatua mbalimbali zinazolenga kuwavutia watalii 850,000 kila mwaka ifikapo mwaka 2025.
Amesema Zanzibar iko wazi kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika michezo ya baharini na fukweni ambayo itaongeza thamani vivutio vya utalii.