Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Bw. Wang Yi, amewafahamisha wanahabari kuhusu ziara yake katika nchi za Ulaya na Russia.
Bw. Wang amemaliza ziara yake nchini Ufaransa, Italia, Hungary na Russia na kuhudhuria Mkutano wa 59 wa Usalama wa Munich.
Bw. Wang amesema kwenye ziara hiyo alifahamisha sera kuu za China baada ya Mkutano wa 20 wa CPC, na kufafanua kwa pande zote mustakbali mzuri na athari za kina za ujenzi wa China ya kisasa.
Kwenye suala la amani na usalama, Bw. Wang amesema China imethibitisha mara nyingi kwa ukweli kwamba njia ya kujiendeleza kwa amani si kama tu inatekelezeka bali pia inafanikiwa.