China kujenga nchi yenye nguvu zaidi ya kilimo kunufaisha dunia nzima
2023-02-24 10:42:43| CRI

Hivi karibuni China ilitoa Waraka Namba 1 kuhusu suala la kilimo, ikiagiza kwa mara ya kwanza kuharakisha ujenzi wa nchi yenye nguvu kubwa ya kilimo. Hatua hii ina umuhimu mkubwa wa kimataifa na itanufaisha dunia nzima.

China kuharakisha kujenga nchi yenye nguvu zaidi ya kilimo kutatoa mchango muhimu kwa mchakato wa kutimiza kilimo cha kisasa duniani. China ni nchi kubwa ya kilimo, na idadi ya watu wlioajiriwa katika sekta hiyo na thamani ya uzalishaji wa kilimo inashika nafasi ya kwanza duniani. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia, mwaka 2019, wastani wa uzalishaji mali kwa mwaka wa kila mtu anayeshughuilikia kilimo nchini China ilikuwa takriban dola 5,609 za kimarekani, ikiwa ni ongezeko la takriban mara 4.87 ikilinganishwa na mwaka 1991, huku wastani wa dunia ukiongezeka kwa takriban mara 1.80 katika kipindi hicho.

Wakati huohuo, kasi ya ongezeko la kiwango cha tija cha kilimo nchini China ilizidi wastani wa kasi hiyo ya dunia kwa asilimia 40. Katika siku za baadaye, China itaharakisha ujenzi wa nchi yenye nguvu zaidi ya kilimo, na kutimiza kilimo wa kisasa, hatua ambayo itachangia zaidi kuharakisha mchakato wa kutimiza kilimo cha kisasa duniani.

Pia, China kuharakisha kujenga nchi yenye nguvu zaidi ya kilimo kutatoa mchango zaidi katika kuhakikisha usalama wa chakula duniani. Mwaka 2021, China ilitoa pendekezo kuhusu maendeleo ya dunia, na kuchukulia usalama wa chakula kama moja ya maeneo nane muhimu ya ushirikiano. Ikiwa na asilimia 9 ya ardhi inayofaa kwa kilimo na asilimia 6 ya rasilimali ya maji safi, China inalisha karibu asilimia 20 ya watu duniani. Hadi kufikia mwaka 2022, China ilivuna  zaidi ya tani milioni 650 za nafaka kila mwaka kwa miaka nane mfululizo. China ni nchi ya kwanza duniani kwa uzalishaji wa nafaka, na nchi ya tatu kwa mauzo ya nafaka kwa nchi nyingine. China itaongeza zaidi uzalishaji wa nafaka, na kuhakikisha usalama wa chakula wa ndani kwa kuboresha ufanisi wa kilimo, kuendeleza teknolojia, na kuboresha mfumo wa usimamizi wa mambo ya kilimo, na itatoa mchango mkubwa zaidi katika kuhakikisha usalama wa chakula duniani.

China kuharakisha kujenga nchi yenye nguvu zaidi ya kilimo pia kutachangia uzoefu wa Kichina kutimiza kilimo cha kisasa duniani. Njia ya kutimiza kilimo cha kisasa ni tofauti katika nchi tofauti. Hivi sasa, kuna njia tatu za kutimiza kilimo cha kisasa duniani: njia ya “kilimo kikubwa” inayotumika nchini Marekani na Canada, njia ya “kilimo kidogo chenye kiwango cha juu” ya Japan na Uholanzi, na njia ya “kilimo chenye thamani ya juu” inayotumiwa na Ufaransa na Italia. Lakini njia hizo zote hazifai kwa China. China ina mamia ya mamilioni ya wakulima, na ni lazima itafute njia maalum ya kutimiza kilimo cha kisasa.

China kuharakisha kujenga nchi yenye nguvu zaidi ya kilimo kutainua kiwango cha ushirikiano wa kimataifa wa kilimo wa China. China ni mshirika mwaminifu wa Umoja wa Mataifa na nchi zinazoendelea katika mambo ya kilimo. Ni nchi inayotoa misaada mingi zaidi, kutuma wataalam wengi zaidi, na kufanya miradi mingi zaidi ya ushirikiano kwa nchi nyingine. Hadi sasa, China imefanya mawasiliano ya teknolojia ya kilimo na zaidi ya nchi 140 duniani, na kutoa zaidi ya teknolojia 1,000 za kilimo kwa nchi zinazoendelea. Kwa mfano barani Afrika, ushirikiano wa kilimo umekuwa sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya China na nchi za bara hilo. Kwa miongo kadhaa iliyopita, China imechangia maendeleo ya kilimo barani Afrika kupitia hatua mbalimbali ikiwemo msaada wa chakula, kuanzisha vituo vya vielelezo vya kilimo, uwekezaji katika kilimo, na kuhimiza mauzo ya bidhaa za kilimo za Afrika nchini China, ambapo imetoa mchango mkubwa katika kuhakikisha usalama wa chakula na kupunguza umaskini barani Afrika. China kuharakisha kujenga nchi yenye nguvu zaidi ya kilimo bila shaka kutaweka msingi imara kwa kuongeza kiwango cha ushirikiano wa kimataifa wa kilimo wa China.