Uchaguzi wa Nigeria waaangaziwa huku ukitarajiwa kuvunja rekodi ya idadi ya wapiga kura
2023-02-24 19:31:44| cri

Watu waliosubiri kwa saa nyingi wamesimama nje ya benki huku wakitarajia kuchukua pesa, siku ya Alhamis huko Lagos, nchini Nigeria. Wapiga kura wanatarajiwa kumchagua kiongozi mpya kesho Jumamosi baada ya Rais Muhammadu Buhari kumaliza muhula wake wa mwisho, ambapo wagombea 18 wanawania kuiongoza nchi hiyo inayokabiliwa na matatizo mengi, hasa uhaba wa pesa taslimu.