Kamati Kuu ya 20 ya CPC yaanza Mkutano wa pili wa wajumbe wote Beijing
2023-02-27 08:53:45| CRI

Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomusti cha China (CPC) imeanza  mkutano wa pili wa wajumbe wote Jumapili mchana hapa mjini Beijing.

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, Xi Jinping aliwasilisha ripoti ya kazi kwa niaba ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu. Mkutano wa Pili wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Chama  utapitia mpango wa rasimu ya mageuzi ya taasisi za chama na serikali, na Ofisi ya Siasa itapendekeza orodha ya majina ya wagombea wa nafasi za uongozi za taasisi za serikali yatakayowasilishwa kwenye  Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China na wagombea wa nafasi za uongozi za Baraza la Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC) kwenye  mkutano wa kwanza wa Baraza la14 la CPPCC.