Russia yaishutumu Marekani kwa kujaribu kuharibu uhusiano kati ya Russia na Afrika
2023-02-27 08:59:16| CRI

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Mikhail Bogdanov amesema Marekani na washirika wake wanafanya kampeni isiyo na kifani ya kuitenganisha Russia katika mambo ya siasa na uchumi, ikiwemo kujaribu kuharibu mkutano wa pili wa wakuu wa Russia na nchi za Afrika unaotarajiwa kufanyika St. Petersburg mwezi Julai.

Bw. Bogdanov amesema tangu mgogoro kati ya Russia na Ukraine uanze, nchi za magharibi zimetoa shinikizo kubwa kwa nchi za Afrika kwa njia kama kuweka vikwazo, kusimamisha misaada ya kifedha na kibinadamu, ili kuharibu uhusiano kati ya Russia na Afrika.