Watu 18 wamejeruhiwa jumamosi baada ya milipuko mitatu kutokea wakati wa mashindano ya mbio za matumaini za Mlima Cameroon zilizofanyika katika mji mkuu wa mkoa wa Kusini Magharibi nchini Cameroon, Buea.
Waziri wa Michezo na Afya ya Mwili wa nchini humo, Narcisse Mouelle Kombi amewaambia wanahabari kuwa, mmoja kati ya majeruhi hao ni mwanariadha na wengine ni watazamaji.
Watu wanaotaka kujitenga na kuunda nchi mpya katika maeneo mawili yanayozungumza lugha ya Kiingereza ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi wamesema kupitia mitandao ya kijamii kuwa, wanahusika na milipuko hiyo.