Timu ya madaktari wa China yatoa mafunzo ya kuondoa uvimbe kwenye ubongo kwa madaktari wa Zambia
2023-02-27 23:10:32| cri

Madaktari nchini Zambia wamefanikiwa kufanya upasuaji kwa watu wanne kuondoa uvimbe katika ubongo baada ya mafunzo yaliyofanywa na kikundi cha 23 cha timu ya madaktari wa China.

Mkuu wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Mafunzo ya Chuo Kikuu nchini Zambia, Kachinga Sichizya amesema, madaktari wa Zambia walifanya upasuaji huo chini ya usimamizi wa mmoja wa madaktari wa China, Chen Zhenbo.

Amesema madaktari wa Zambia, wamejiandaa kwa upasuaji huo kwa miezi miwili iliyopita, na kuongeza kuwa, mafanikio ya upasuaji huo ni ishara kuwa madaktari wa Zambia sasa wanaweza kufanya upasuaji huo baada ya madaktari wa China kuondoka nchini humo mwezi ujao.