Watu watano wakiwemo wanawake wawili na wanaume watatu, wamejeruhiwa kufuatia watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa kundi la Boko Haram kulipua mabomu ya lami toka Milima ya Mandara ya Gwoza, iliyopo eneo la serikali ya mtaa wa Jimbo la Borno wakiwalenga wapiga kura.
Washambuliaji hao wanahisiwa kutoka kwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika kambi ya Ali Ngulde, na walifanya mashambulizi wakati wapiga kura wakikaribia kuanza mchakato wa upigaji kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge uliofanyika nchini humo jumamosi iliyopita.