China yasema itachangia katika uongozi wa haki za binadamu duniani
2023-02-28 09:37:52| CRI
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amesema, China itafuata nia yake ya maendeleo ya haki za binadamu na kutoa mchango katika uongozi wa haki za binadamu duniani.
Qin Gang amesema hayo alipohutubia mkutano wa ngazi ya juu wa 52 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video. Amesema nchi zinapaswa kushikilia njia ya maendeleo ya haki za binadamu ambazo zinaendana na mazingira ya taifa husika.
Amesema suala la haki za binadamu nchini China limepata mafanikio makubwa katika historia kutokana na nchi hiyo kufuata njia inayoendana na mwelekeo wa wakati na inayoendana na mazingira ya nchi hiyo, na amesisitiza kuwa, China inapinga kithabiti majaribio ya kutumia masuala yanayohusiana na Xinjiang na Tibet kuchafua taswira ya China na kuzuia maendeleo yake.