Mkutano wa pili wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya CPC watoa taarifa
2023-03-01 09:41:47| CRI

Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) jana Jumanne ilitoa taarifa mwishoni mwa mkutano wake wa pili wa wajumbe wote.  

Xi Jinping ambaye ni rais wa China na katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, alitoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo wa siku tatu ambao uliongozwa na Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC.

Wakati wa mkutano huo, kamati kuu ya CPC ilisikiliza na kujadili ripoti ya kazi iliyowasilishwa na rais Xi. Mkutano huo pia umepitisha orodha ya wagombea waliopendekezwa kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi kwenye taasisi za serikali, pamoja na orodha ya wagombea wa nafasi za uongozi za Kamati ya Ushauri wa Kisiasa ya China (CPPCC) ili kujadiliwa kwenye kikao cha kwanza cha Bunge la 14 la Umma la China NPC na kikao cha kwanza cha awamu ya 14 ya CPPCC.

Kwa mujibu wa taarifa mkutano huo pia umepitisha mpango wa mageuzi ya taasisi za Chama na serikali.