Kamati Kuu ya CPC yafanya mkutano wa mashauriano juu ya mpango wa mageuzi ya taasisi za Chama na serikali
2023-03-01 09:40:19| CRI

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) jana Jumanne ilifanya mkutano wa mashauriano ili kusikiliza maoni na kuwajulisha wanachama wasio wa CPC, Shirikisho la Viwanda na Biashara la China (ACFIC) na watu wasiojihusisha na chama, juu ya mpango wa mageuzi ya taasisi za chama na serikali pamoja na orodha ya wagombea waliopendekezwa kushika nyadhifa za uongozi kwenye taaasisi za serikali.

Akitoa hotuba kwenye mkutano huo, rais wa China na katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping amesema, Mkutano Mkuu wa 20 umeweka mipango mikubwa juu ya mageuzi ya kina ya taasisi za Chama na serikali, ukiwa na maelekezo ya wazi kuhusu kazi husika, ikiwemo kuimarisha mageuzi ya muundo kwenye sekta ya fedha na kuboresha mfumo ambao kamati kuu ya Chama itatekeleza uongozi wa pamoja kwenye kazi ya sayansi na teknolojia miongoni mwa nyingine.

Rais Xi amesema duru hii ya mageuzi ya taasisi za chama na serikali inaangazia sekta na nyanja muhimu, na kulenga kuondoa matatizo magumu yanayohusiana na umma, na kutarajiwa kuleta matokeo makubwa kwenye uchumi na maendeleo ya jamii.