Watu wenye silaha wawateka nyara vijana 25 kaskazini mwa DRC
2023-03-01 18:20:41| cri

Watu wenye silaha wasiojulikana wamewateka nyara vijana 25 kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa mashambulizi dhidi ya vijiji kadhaa katika eneo hilo.

Ofisa wa serikali ya mtaa Marcellin Mazale Lekabusiya amesema watu hao walivamia vijiji vitatu katika eneo la Banda katika jimbo la Bas-Uele Jumanne asubuhi na kuwateka nyara watu 25 wenye umri wa kati ya miaka 12 na 18. Saba kati ya waliotekwa nyara walikuwa wasichana.

Eneo la kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekuwa na amani kwa muda mrefu, lakini limekuwa likisumbuliwa kidogo na ghasia za wapiganaji ambazo zimelikumba eneo la mashariki mwa nchi hiyo kwa miongo kadhaa.