Kiongozi wa Sudan asema yuko tayari kuimarisha ushirikiano na Sudan Kusini
2023-03-01 09:39:41| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan amesisitiza kuwa nchi hiyo inapenda kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na Sudan Kusini.

Al-Burhan aliyasema hayo jana Jumanne alipokutana na mshauri mkuu wa rais wa Sudan Kusini anayeshughulikia Mipango Maalum Benjamin Paul mjini Khartoum.

Bw. Paul pia alikabidhi salamu za maandishi kutoka kwa Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili jirani.

Pia siku hiyohiyo, mshauri wa usalama wa rais wa Sudan Kusini Tut Gatluak alifanya ziara mjini Khartoum. Alisema, Sudan Kusini ina nia ya kudumisha amani na utulivu nchini Sudan ikiwa kama kuongeza zaidi utulivu nchini Sudan Kusini. Kwa mujibu wa Gatluak, wakati Sudan ikifuata Mkataba wa Amani Uliotiwa saini 2018 ili kuhakikisha amani endelevu nchini Sudan Kusini, Sudan Kusini pia imefuata Mkataba wa Juba wa Amani ili kuhakikisha utulivu wa Sudan

Sudan Kusini ilisaidia kupatanisha Mkataba wa Amani wa Juba uliosainiwa kati ya serikali ya mpito ya Sudan na makundi kadhaa yenye silaha mnamo Oktoba 3, 2020 ili kumaliza vita vilivyodumu miaka mingi.