Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) imetoa taarifa ikisema wataalamu wametoa wito kwa nchi za Afrika kuziba pengo lililopo la kiteknolojia katika bara zima ili kurahisisha mageuzi ya nishati.
Wito huo umetolewa kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu ya sera katika Kongamano la 5 la Sayansi, Teknolojia, na Ubunifu la Afrika kuhusu Teknolojia za Nishati Zinazoibuka ambayo yalikutanisha wataalamu wa Afrika na Umoja wa Mataifa Februari 26 na 27 huko Addis Ababa, Ethiopia.
Wataalamu hao walitoa wito wa kufanya marekebisho ya kina barani Afrika katika masuala ya nishati ili kuondoa mzunguko mbaya wa teknolojia zilizopitwa na wakati, na kukabiliana kwa ufanisi zaidi na mahitaji ya umeme na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha ECOWAS cha Nishati Mbadala na Ufanisi wa Nishati Bw. Francis Sempore, haidrojeni ya kijani katika Afrika Magharibi inaonekana ni ndoto kwa sasa, lakini hata uamuzi wa viongozi wa ECOWAS wa kupitisha sera ya kikanda ya nishati mbadala mwaka 2013, kwani bado ni jambo lisilofikirika kwa nchi kutokuwa na nishati ya jua katika mchanganyiko wake wa nishati.