Kenya kuunga mabasi 130 ya umeme kutoka China mwaka 2023
2023-03-01 19:18:34| cri

Kampuni ya Associated Vehicle Assemblers ya nchini Kenya (AVA) imesema, itaunga mabasi 130 ya umeme yaliyotengenezwa na kampuni ya magari ya China ya BYD katika mwaka 2023.

Mkurugenzi Mtendaji wa AVA Matt Lloyd ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua huwa, mpaka sasa tayari kampuni hiyo imeunga mabasi 15 ya umeme yaliyotengenezwa na kampuni ya BYD kwa ajili ya soko la ndani la Kenya.

Amesema faida ya kutumia kampuni ya BYD ni kwamba hii ni moja ya kampuni zinazoongoza katika utengenezaji wa magari ya umeme na ngazi ya ubora wa magari hayo ni ya juu sana.