UNHCR yatafuta fedha zaidi kukabiliana na mgogoro wa kibinadamu nchini Somalia
2023-03-02 14:44:51| cri

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetoa wito wa fedha zaidi ili kudumisha misaada ya kibinadamu nchini Somalia, ambayo imekumbwa na ukame mkali.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Magatte Guisse amesema, fedha zilizopo zinaweza kujibu mahitaji ya kibinadamu kwa mwezi Machi pekee. Amesema kwa saa wameweza kukwepa baa la njaa, lakini mahitaji bado ni mengi na ya dharura, huku zaidi ya moja ya tatu ya idadi ya watu nchini Somalia wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, na karibu nusu ya watu nchini humo wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Somalia inashuhudia miaka mitano ya uhaba wa mvua, hali ambayo haijaonekana katika miaka zaidi ya 40 iliyopita, na msimu wa sita wa uhaba wa mvua unatarajiwa kuzifanya familia zaidi kukimbia makazi yao.