China yasaidia Watoto wa Kenya kutimiza ndoto ya Masomo
2023-03-02 10:43:24| CRI

Karibu tena msikilizaji katika kipindi hiki cha DARAJA kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo msikilizaji tutakuwa na habari mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika, pia tutakuwa na ripoti kuhusu China inavyowasaidia watoto nchini Kenya kutimiza ndoto zao za kielimu, na tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi, na yatazungumzia wanafunzi wawili kutoka shule ya upili ya MCEDO Beijing waliofanya vyema kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne mwaka uliopita, na kupata ufadhili wa kuja China kuendelea na masomo yao.