Kampuni za China, Saudi Arabia zafungua kiwanda cha kuunganisha mabasi nchini Misri
2023-03-02 20:47:44| cri

Kiwanda kipya cha kuunganisha mabasi kilichojengwa kwa pamoja na makampuni ya China na Saudi Arabia kimeanza uzalishaji katika mji wa New Suez nchini Misri, huku kundi la kwanza la mabasi likitarajiwa kuanza kuunganishwa hivi karibuni.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Jumanne, mwenyekiti wa kampuni ya Saudi Arabia ya ATM Misr Bw. Hamed Al Mutabagani, amesema kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha mabasi 500 kwa mwaka, na kitakuwa katika eneo la mita za mraba 164,000 na kina vifaa vya kisasa vya uzalishaji, ghala, na vifaa vya kudhibiti ubora.

Kampuni hizo za Misri na Saudi Arabia zinashirikiana na kiwanda cha mabasi cha China King Long.