Takwimu mpya zilizotolewa jana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) zimeonyesha kuwa, wakati mabilioni ya watu duniani hawawezi kupata lishe kamili, gharama ya lishe hiyo inatofautiana sana kati ya maeneo.
Shirika hilo limetoa takwimu hizo kutokana na utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia pamoja na Chuo Kikuu cha Tufts cha Marekani, kwa kushirikiana na wachambuzi wa Shirika hilo.
Ripoti hiyo imeonyesha kuwa, gharama ya lishe bora katika sehemu kubwa ya Amerika ya Kusini na Caribbean kwa siku kwa mwaka 2020 ilikuwa ni dola za kimarekani 3.89 kwa mtu, huku Asia ikichukua nafasi ya pili kwa dola za kimarekani 3.72. Bara la Afrika, gharama ya lishe bora ilikuwa ni dola za kimarekani 3.42 kwa mtu kwa siku, na Amerika ya Kaskazini na Ulaya ni dola za kimarekani 3.19 na Oceania ni dola 3.07 za kimarekani.