Xi avitaka vyuo vya Chama kuendelea kujitolea katika kulea vipaji na kuchangia busara
2023-03-02 14:18:43| CRI

Rais wa China na katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Xi Jinping, amevitaka vyuo vya Chama kuendelea kujitolea kwenye kazi ya uanzilishi ya kulea vipaji na kutoa mchango wao wa busara kwenye Chama.

Kauli hiyo ameitoa wakati akihutubia mkutano wa kuadhimisha miaka 90 ya kuanzishwa kwa chuo cha chama cha CPC na sherehe ya ufunguzi wa muhula mpya wa mwaka 2023.

Ameeleza kuwa vyuo vya chama katika ngazi zote ni lazima vizingatie kazi kuu na kutumikia maslahi ya jumla ya nchi, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuambatana na mwelekeo sahihi katika kuendesha vyuo vya chama na vilevile kuvitaka kulinganisha fikra zao, msimamo wa kisiasa na vitendo na Kamati Kuu ya CPC.

Aidha rais Xi amevitaka vyuo hivyo kubeba wajibu mkubwa katika kulea maafisa wakuu wa serikali ambao wataweza kubeba kazi ya kuhuisha taifa.